FUNDI UMEME HATIANI KWA KUTOA RUSHWA, SOMA MKASA WOTE HAPA


NA MWANDISHI WETU, KINONDONI.

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kinondoni imemhukumu Fundi Umeme Bw. SAID NASIBU KILANGA  adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya sh. Laki mbili (200,000) baada ya kukutwa na hatia katika kosa la kutoa rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) & (2) cha Sheria ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa namba 329 Rejeo la 2022.


Hukumu dhidi ya Bw. Said Nasibu Kilanga imetolewa Julai 31, 2024 kutokana na shauri la jinai namba 218/2023 lililokuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Nabwike Mbaba, shauri ambalo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya ya Kinondoni Bw. Aidan Samali 


Ilielezwa kuwa Mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Septemba 5, 2023 kwa shtaka tajwa hapo juu ambapo mshtakiwa  alitoa rushwa kiasi cha sh 50,000/= kwa Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mburahati Bw. Yusuph Nammohe ili amsaidie kumaliza tuhuma za wizi wa mtandaoni zilizokuwa zikimkabili kituoni hapo.


Mahakama katika hukumu yake imemkuta mshtakiwa na hatia na kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani au kulipa faini ya sh. Laki mbili (200,000) ambapo mshtakiwa amelipa faini hiyo.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA