WAAJIRI HALMASHAURI ZA MKOA WA MWANZA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA TALGWU


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana amewataka Wakurugenzi na Maafisa rasilimali watu wa Halmashauri za Mkoa wa Mwanza kudumisha mahusiano na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) ili kuboresha Utendaji kazi na kutatua changamoto za Wafanyakazi sehemu za kazi kwani zinategemeana.

Hayo yamesemwa leo katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kati ya Viongozi wakuu wa Chama na waajiri hao kuhusu masuala mbalimbali ya vyama vya wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kingdom Jijini Mwanza.


Ndg. Balandya Elikana alisema mafunzo haya yaliyoandaliwa na TALGWU ni muhimu kwani yanamrengo wa kubadilishana uzoefu kwa pande hizo mbili kwa namna ya kuhudumia Wafanyakazi.

"Vyama vya Wafanyakazi ni muhimu kuwezeshwa ili viweze kuwa imara kwa ajili ya kusimamia haki na maslahi ya Wafanyakazi", alisema.

Ndg. Elikana alisisitiza kwamba endapo mahala pa kazi patakuwa na Chama imara ambacho kinapewa nafasi na waajiri kutekeleza majukumu yake basi Chama hiko kitasababisha kuwepo kwa amani na utulivu na amani mahala pa kazi na Watumishi nao watatoa huduma bora kwa wananchi na kuleta tija katika nchi.

Aidha Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Balandya Elikana alisema Serikali ya Mama Samia inapiga vita uzembe kazini hivyo ameitaka TALGWU kuendelea kuhimiza Wanachama wake kufanya kazi kwa bidii, maarifa na uzalendo ili kusogeza mbele maendeleo ya nchi. 

Pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuwapa nafasi ya kujiendeleza Watumishi ili waendane na kasi ya mabadiriko ya teknolojia.

Alimalizia kwa kuwataka Wakurugenzi na mafisa rasilimali watu waliohudhuria mafunzo hayo watumie fursa hiyo vizuri kwa kubadilishana uzoefu ili mafunzo hayo yawe nyenzo muhimu katika kuboresha mahusiano baina ya Chama na Waajiri ili pande zote mbili ziweze kufanya kazi kwa maslahi ya Wafanyakazi.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TALGWU Taifa Ndg. Tumaini P. Nyamhokya aliwaomba waajiri hao kufanya kazi kwa ukaribu na Chama ili kuepusha migogoro kazini. Aidha aliwataka kufuata sheria katika kufanya kazi na vyama ili kuondoa migogoro inayojitokeza hivi sasa kati ya Chama kimoja cha Wafanyakazi na kingine.


Katibu Mkuu wa TALGWU Ndg. Rashid M. Mtima alisema mafunzo haya yameandaliwa mahsusi kabisa ili kujenga uelewa wa pamoja wa dhana ya uwepo wa TALGWU mahala pa kazi pamoja na kuboresha mahusiano kati ya waajiri na Chama. Alisema mafunzo hayo yatatolewa nchi nzima ambapo tunategemea mara baada ya mafunzo haya inategemewa kuonekana mahusiano kati ya Chama na waajiri yameboreka na kuleta tija mahala pa kazi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa TALGWU Taifa Ndg. Tumaini P. Nyamhokya akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Katibu Mkuu wa TALGWU Ndg. Rashid M. Mtima akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Katibu Mkuu wa TALGWU Ndg. Rashid M. Mtima akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Naibu Katibu Mkuu wa TALGWU Ndg.Wandiba Kongoro akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Katibu wa Mkoa wa Mkoa wa Mwanza, Hosea Yusto akizungumza wakati wa mafunzo hayo

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA