KINANA AKEMEA WANAO PITAPITA KABLA YA MDAA

 

                Na, Ernest Makanya - Mara


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara ndugu Abdullahman Kinana amewataka viongozi wa Chama hicho Mkoa wa Mara kutokubeba wagombea au kupandikiza wagombea kwa njia yoyote kuelekea Chaguzi mbili za Serikali za Mitaa zinazotarajiwa kufanyika mapema August 2024 na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025


Kinana ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri iliyoboreshwa Wilaya ya Tarime leo April 14, 2024 akiwa katika ziara ya kikazi hasa kwa kuzingatia yeye ni Mlezi wa Mkoa wa Mara.


Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya Viongozi ambao wamekuwa wakitoa rushwa kupata uongozi ikiwemo viongozi wanaopekea rushwa ambapo amesistiza vitendo vya rushwa vinasababisha kupata viongozi wanaoshindwa kuitumikia jamii.

Naye Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini Mhe. Mwita Waitara ameshiriki ziara hiyo ambapo pia amepata nafasi ya kutoa neno na kuwataka watu wasipotoshe juu ya pesa za CSR pia ameweka wazi kuwa kile kinacho fanyika Nyamongo sio kanuni yake bali ni kanuni ya serikali  inayo simamia pesa za CSR hivyo asitokee mtu akawapotosha na kuwataka kama wana malalamiko basi wawasilishe ili wasikilizwe.


"Toka nimekuwa Mbunge jambo ambalo limetumia muda mwingi ni CSR na limekuwa linapotoshwa sana na tumekaa sana kwenye huu ukumbi kujadili jambo moja na wamekuja viongozi mbali mbali hapa akiwemo Afisa madini wa Mkoa tumeenda ziara sehemu mbalimbali kama Geita lakini tukirudi wanajadili jambo hilo hilo  na wanasema hii kanuni ni ya Waitara mimi nataka kuwambia kuwa hiyo sio kanuni yangu ni kanuni ya serikali na nimewaambia kama kuna sehemu haiko sawa leteni mapendekezo tuyawasilishe “Amesema Waitara “ 


Maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025 tayari yameanza Hivyo Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho amewakumbusha wana CCM kote nchini wakiwemo wa Mkoa wa Mara kutenda haki katika chaguzi huku akisisitiza kuchagua na kuchaguliwa ni haki ya kila mtu.








Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA