SERIKALI ITAENDELEA KUFANYA MATENGENEZO YA BARABARA MOSHI VIJIJINI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali itaendelea kufanya matengenezo ya barabara katika Zahanati ya Mawela ili kurahisisha utoaji huduma kwa Wananchi wa Moshi Vijijini kama ilivyokusudiwa.


Mhe. Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, aliyeuliza Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kisomboko kwenda Zahanati ya Mawela, Moshi Vijijini kwa kiwango cha changarawe?


Amesema inakadiriwa kuwa na Kilomita 3 ya barabara hiyo ambayo haijasajiliwa katika mtandao wa barabara zinazohudumiwa na Tarura, barabara hiyo ni moja kati ya barabara zinazoelekea  Zahanati ya Mawela ikiwa ni pamoja na barabara ya Uru Seminari, Kifunguni ambayo ni Kilomita 4.5 na Murangi, Kisalika High School  ambayo ni Kilomita 3 ambayo kwa mwaka 2024/2025 itafanyiwa matengenezo ya kawaida  kwa gharama ya Shilingi Milioni 900.


Mhe. Katimba amesema mwaka 2024/2025 Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Wananchi wa maeneo husika itahakikisha barabara ya Kisomboko, Zahanati ya Mawela inafanyiwa matengenezo ili iweze kupitika na kutoa huduma.


Aidha Mhe. Katimba amesema katika mwaka wa fedha  2024/2025 barabara ya Mawela Kanisani kwenda Zahanati ya Mawela itafanyiwa matengenezo ili iweze kupitika na kutoa huduma iliyokusudiwa kwa Wananchi. 


 “Tayari vikao hivyo vimeshaketi tarehe 13, Novemba 2023 kikao cha bodi ya barabara ya Mkoa ilikaa na kupitisha barabara zenye urefu wa Kilomita 413 ni maombi ya kwa ajili ya kupitishwa ili yaweze kuingia katika mtandao utakao hudumiwa na Tarura, Serikali inachukua hatua barabara hizi tayari zimeshapitishwa kwenye utaratibu bado kudhibitishwa ili zianze kuhudumiwa na Tarura" Mhe. Katimba


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA