WIZARA YA ELIMU YAOMBA KUPITISHIWA ZAIDI YA TSH. TRILIONI MOJA YA BAJETI 2024/25

 


Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia imeliomba Bunge kuidhinishiwa jumla ya Tsh.Trillioni Moja, Bilioni Mia tisa Sitini na Nane, Milioni mia mbili kumi na nane na elfu Mia tano na thelathini na nne (1,968,218,534,000.00.) ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/ 2025.


Ombi Hilo limewasilishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Waziri Prof.Adlf Mkenda alipowasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo amesema ili kuwezesha utekelezaji wa malengo kwa mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Fungu 46) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,965,330,380,000.00 kwa mchanganuo ufuatao:


“Shilingi 637,287,706,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara ambapo Shilingi 585,225,031,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi 52,062,675,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo; na Shilingi 1,328,042,674,000.00 zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 1,033,393,669,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 294,649,005,000.00 fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo." Pro. Mkenda

"Wizara kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO (Fungu 18) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,882,154,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Mishahara ni Shilingi 1,319,040,000.00 na Matumizi Mengineyo ni Shilingi 1,563,114,000.00." Prof. Mkenda


"Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa naomba sasa Bunge lako tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara (Fungu 46 na Fungu 18) yenye jumla ya Shilingi 1,968,212,534,000.00.”ameeleza Waziri Prof. Mkenda


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA