TRA YATOA ELIMU YA KODI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO SHINYANGA

Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga imetoa elimu ya Kodi kwa Wanafunzi wanachama wa Vilabu vya Kodi kutoka shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo na ufahamu wa masuala mbalimbali ya kodi.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Mei 10,2024 katika Ukumbi wa Makindo Hotel Mjini Shinyanga yakishirikisha wanafunzi kutoka shule ya Msingi Little Treasures, Shule za Sekondari Old Shinyanga, Uhuru na Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy Com) na Chuo cha St. Joseph.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea ufahamu wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali ya kodi.

“Mafunzo ambayo tunayaandaa yanalenga kuwafundisha vijana wetu wakiwa wadogo hasa wanafunzi wa shule za Msingi, Sekondari na vyuoni kujua maana ya kulipa kodi, umuhimu wa kodi ni nini, kwanini serikali zote duniani zinaweka kodi. Kodi ni malipo ya lazima ambayo mwananchi mzalendo anatozwa kwa ajili ya kuisaidia serikali yake iweze kuendesha majukumu yake kwa wananchi”,amesema David.

“Ni muhimu sisi wananchi kuhakikisha tunapokwenda kupata huduma yoyote tupewe risiti ya EFD na wafanyabiashara watoe Risiti. Na nyinyi ni mabalozi wazuri kwa sababu msingi mzuri kwa sababu tunaamini tukiwafundisha mngali wadogo mtakuwa wazalendo wazuri wa nchi hii”,ameongeza.

Kwa upande wake, Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi amesema kodi ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya taifa, inasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi, ujenzi wa miundombinu na huduma za kijamii hivyo kuwashauri wafanyabiashara kujisajili TRA ili wapate namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN), kufanyiwa makadirio ya kodi kila mwaka, kuwasilisha Return na kulipa kodi sahihi na kwa wakati sahihi.

Nao wanafunzi kutoka Vilabu vya kodi wameishukuru TRA kwa kuwapatia elimu ya masuala ya kodi na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa kueneza elimu hiyo kwa jamii ili kuhakikisha kila mwananchi anawajibika kulipa kodi.
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 10,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga
Afisa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Joel Elias akitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA