TANESCO NA ZESCOKUENDELEZA UJENZI WA NJIA YA UMEME KUUNGANISHA TANZANIA, ZAMBIA


Tarehe 25 Oktoba 2023 Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Mha.Gissima Nyamohanga akiwa sehemu ya washiriki katika Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Zambia, alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la umeme la Zambia ZESCO Victor Benjamin Mapani kuhusu ushirikiano wa kikazi kati ya mashirika haya mawili.

Katika mazungumzo yao waliongelea maendeleo ya ujenzi wa njia ya 330kV inayotoka Tunduma kwenda Nakonde ili kuunga nchi hizi mbili kwenye EAPP na SAPP.

Pia, waliongelea mpango wa Zambia kununua umeme kutoka Tanzania kiasi cha 400MW pamoja na uwezekano wa Zambia ikishirikiana na Tanzania kujenga Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia upande za Tanzania ambacho itapeleka umeme Zambia.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA