RAIS SAMIA AMETOA DIRA NA KUWEZESHA UTEKELEZAJI WA MAONO - WAZIRI PROF. KITILA MKUMBO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa maono na  kutoa Dira ili watu kufanya makubwa kutokana na staili yake ya Uongozi.

Ameyasema hayo Leo Septemba 20, 2023 wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Vioo vya Ujenzi cha Saphire float Glass kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani.

Amesema Kazi kubwa ya kiongozi ni kutoa Dira na maono na kuwezesha utekelezaji wake, kwani kiongozi mashuhuri sio yule anayefanya makubwa bali ni yule anayewezesha watu kufanya makubwa.

"Hakuna shaka kwamba kwa Staili yako ya Uongozi unaendelea kujijengea umashuhuri Mkubwa kupitia maono haya mawili, kwanza umetoa maono na dira yako wazi kabisa, Pili umewezesha utekelezaji wa Maono na Dira yako kutekeleza kikamilifu na mifano ipo tele ikiwemo uwekezaji" Alisema Waziri Prof. Kitila

Akizungumzia kuhusu Uwekezaji huo amesema ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi kama ambavyo inaelekeza kujenga uchumi wa kisasa, shirikishi na shindani huku msingi wake ukiwa ni viwanda, utakaowezesha ustawi wa wananchi.     

Waziri Prof. Kitila amesema Rais Samia Suluhu Hassan wakati akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza mnamo April 22, 2021 alieleza Dira ya Serikali ya awamu ya Sita  kuwa " Dira na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya Sita itakuwa ni kudumisha mazuri ya awamu zilizopita, kuyaendeleza mema yaliyopo na kuleta mapya." Alisema Waziri Kitila.

Aidha, amesema Rais Samia amedhihirisha kwamba analeta mapya kupitia kiwanda hicho ambacho Serikali inatarajia kupata mapato Mapya ya Kodi ya Tsh. Bil 42.79 kwa Mwaka na unatarajiwa kuingiza Fedha za Kimarekani na itasaidia kuokoa Fedha za Kigeni ambazo zimekuwa zikitumika kila mwaka kuagiza bidhaa ambazo kwa sasa zitakuwa zinazalishwa katika kiwanda hicho.

Kwa upande wa Ajira,  Prof. Kitila amesema Kiwanda hicho kimeshaajiri watu 750 na kati ya hao asilimia 49 ni Mafundi na Waendeshaji huku asilimia 39 ni Mafundi wasiohitaji Ujuzi Maalum.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA